KASI YA UJENZI WA BOMBA LA MAFUTA YAMUINUA BALOZI KISESA

Опубликовано: 11 Сентябрь 2024
на канале: Mwananchi Digital
4,213
32

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Meja Jenerali Paulo Kisesa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima hadi Tanga, ambapo asilimia 50 ya mabomba tayari yanaendelea kutandazwa.

Alisema hayo alipotembelea kituo cha Chongoleani mkoani Tanga na kuwapongeza wakandarasi wa mradi huo.

Msimamizi wa Kambi ya Chongoleani, Reni Bezian wa kampuni ya DOCG, amesema wamefikia asilimia 20 ya utekelezaji wa mradi, ikiwemo ujenzi wa mapipa manne yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni nne za mafuta. Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Jafar Kubecha, ameahidi kuendelea kulinda mradi huo na kutoa msaada kwa wakandarasi pale inapohitajika.