HII HAPA RATIBA MAZISHI YA PADRI ALIYEFARIKI KWA AJALI MWANGA 'ATAZIKWA MANYONI'

Опубликовано: 11 Сентябрь 2024
на канале: Mwananchi Digital
3,678
9

Paroko wa Parokia ya Mkula, jimbo la Ifakara, mkoani Morogoro, Padri Nicolaus Ngowi aliyefariki dunia katika ajali ya gari juzi jioni atazikwa Jumatano ya Septemba 17, mwaka huu kwenye makaburi ya wamisionari wa Damu Azizi ya Yesu, yaliyopo Manyoni, mkoani Singida.

Padri Ngowi alifariki papo hapo, Septemba 9, 2024 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Kiruru Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari lake aina ya Toyota Prado alilokuwa akiliendesha kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Kilenga.

Padri Ngowi alikuwa akitokea Ifakara mkoani Morogoro akielekea nyumbani kwao Marangu mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kuhudhuria shughuli ya kifamilia iliyokuwa ifanyike Jumanne Septemba 10, 2024.

Akizungumza na Mwananchi leo jijini Dodoma, Mkuu wa Shirika la Damu Azizi ya Yesu, Tanzania, Vedasto Ngowi amesema maziko ya padri huyo yatafanyika Jumanne Septemba 17, mwaka huu Manyoni mkoani Singida