#MWANZA #UCHAWI #MAGU
Jeshi la polisi wilayani Magu mkoani Mwanza limefanikiwa kumuokoa kwenye mikono ya wananchi wenye hasira kali mama mmoja anayefahamika kwa jila la Salome James mkazi wa kijiji cha Sato anayedaiwa kuwafanya misukule baadhi ya wakazi wa kijiji hicho na kuwatumikisha kwenye mashamba yake,
Kijana Shija Peter ni mmoja kati ya waliopotezwa na kufanywa msukule kwa muda wa miezi minne na mama huyo amesema alikuwa analazwa sehemu moja na fisi huku akiishia kunyweshwa uji huku familia yake ikiwa haijui mahali alipo,
Seko nyabanya ni Mganga wa jadi aliyefanikiwa kumtoa katika hali ya msukule kijana Shija Peter anaeleza hali aliyokuwa nayo kijana huyo kabla na baada ya kumrudisha katika hali yake ya kawaida na kuweza kujitambua,

Hali hiyo ikapelekea mkuu wa wilaya hiyo ya magu ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kumuagiza mkuu wa polisi wa wilaya kumchukua mama huyo kwa ajili ya mahojiano ikiwemo na kumnusuru na hasira za wakazi hao.