Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Halima Bulembo amesema si jambo la busara wabunge wa upinzani kupinga uamuzi wa Serikali wa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na ujenzi wa reli ya kisasa kwa maelezo kuwa hata katika Ilani ya Uchaguzi ya Chadema na ACT-Wazalendo za mwaka 2015, zimezungumzia uendelezaji wa maeneo hayo.