Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao.