MAJONZI: Mazishi ya Aliyekufa siku ya Ndoa, Yatikisa Moshi!

Опубликовано: 01 Январь 1970
на канале: Global TV Online
147,299
355

MAJONZI: Mazishi ya Aliyekufa siku ya Ndoa, Yatikisa Moshi!

ARUSHA! Inasikitisha sana! Mazishi ya bwana harusi, Heaven Makupa (47) aliyefariki dunia katika kanisa Yesu ni Nuru Ya watulililopo Olmatejoo jijini Arusha, yametikisa mjini Moshi kutokana na tukio hilo lilivyogusa hisia za wengi.

Makupa alipatwa na umauti huo hivi karibuni katika kanisa hilo wakati akijiandaa kufunga ndoa na mkewe mtarajiwa, Jeni Kimaro.

Mara baada ya kufariki, mwili wake ulihifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru ambapo asubuhi ya jana Januari 02, wanandugu waliuchukua mwili huo na kwenda nao Marangu Mamba Kokirie mjini Moshi kwa ajili ya mazishi.

Awali kabla ya mazishi umesomwa Wasifu wake ambapo umetaja kuwa alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la juu la damu ambalo ndilo lililogharimu uhai wake na ameacha mke na watoto wawili.

Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw
Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL
Website: www.globalpublishers.co.tz

FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers
Instagram: www.instagram.com/globalpublishers
Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari

Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV
Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho

Jiunge na familia ya Global TV- Club https://goo.gl/mkvuoB