MWANAMKE AGAAGAA KWENYE VUMBI KISA KUIONA BARABARA YA CHANGARAWE

Опубликовано: 01 Январь 1970
на канале: MZAWA TV Online
139
1

#mzawatv
Kutokana na kilio cha miaka mingi juu ya miundombinu mibovu ya barabara iliyokuwa ikikwamisha shuguli za maendeleo pamoja na kukosa huduma za afya kwa wakati katika kijiji cha Ligumbilo wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe,wananchi hao kwa sasa wameondokana na changamoto hiyo baada ya serikali kuwajengea barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi Mil.114 kwa kiwango cha changarawe.

Barabara ya Mlangali - Ligumbilo inaelezwa kuhudumia wakazi zaidi ya 8,500 wa vijiji vitatu ambavyo vimeunganishwa na barabara hiyo ambapo ni kijiji cha Itundu, Lifumbu na Lugumbilo ambayo imetengenezwa kwa urefu wa Km.7.8 na tayari imekwisha kamilika kwa asilimia 100 na kukabidhiwa kwa wananchi ambapo baadhi yao akiwemo Julieta Mkalawa wameonyesha furaha yao kwa kugaagaa kwenye barabara hiyo.
...........
Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii
►YOUTUBE:    / @mzawatvonline  
►INSTAGRAM:   / mzawa  
►TWITTER:   / mzawablog_  
►FACEBOOK:   / mzawabog  
►WEBSITE: https://mzawa.co.tz/